Uenda ukajiuliza maswali mengi kuhusiana na wadogo zetu,hivi wadogo zetu wanaweza kukwazikaje na kukerwa na mambo yetu wakubwa zao?pamoja na kwamba anaweza kutoa kutoka wazazi pia kuna mambo watoto wanaweza kuiga(imitate) kutoka kwa kaka,dada,mama,baba au jamii inayomzunguka na mazingira yanayomzunguka(Nature influence/environment influence) mfano mtoto anaweza kuanza kuongea lugha(language development) mapema kutoka kwa wazazi (biological heritage) au kutokana na jamii inayomzunguka(external influence).   Tuwaonye wadogo zetu pale tunapoona uzembe katika kazi na wanapoonesha sifa mbaya kwa jamii yake.     Tuwape kazi kulingana umri/uwezo wao hii ni kama motisha kwao na kuwafanya wafanye vizuri.    Tusioneshe dalili yoyote yakumpendelea mtoto au baadhi ya watoto na huku wengine unawapuzia.   Tuwape motisha(reinforcement) pindi wanapofanya vizuri au wapokaribia kufanya vizuri,mfano hongera jeni umepiga vizuri deki kesho ntakununulia gauni zuri sana.   Tuwashirikishe katika kazi tunazoziendesha ili kumpa mtoto maarifa na kujifunza toka kwako,sababu wadogo zetu wanaiga mambo toka kwetu.   Tupunguze adhabu kali ambazo zitamfanya mtoto kukuogopa na kumsabisha ashindwe kuiga au kujifunza mambo mengi muhimu kutoka kwako.   Tuwafundishe maadili mema,wewe kama mtu mzima fanya jambo jema popote au muda wowote ili kuonyesha maadili mema na kuwazesha wadogo zetu kujifunza toka kwetu,hepukana na mambo ambayo yaweza kushushia cv (heshima) yako na kusababisha wadogo zetu kuiga hiyo tabia mbaya.   Hayo ni baadhi ya mambo machache yakufanya kwa wadogo zetu,pia mambo yanaweza yakatumiwa na wazazi wetu kwetu,pia nasi kwa watoto zetu.Ahsanteee!!!!!

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Dear members,

If you wish it, you can support your forum by doing a donation, and become an actor of this forum.
All your donations will guarantee the continuity and the quality of this forum.

Your administrator.

Note: Please fill out the fields marked with an asterisk.